Beib Alikuwa Akilipa Bili Nilipokuwa Nimesota, Ferdinand Omanyala Asema

Publish date: 2024-07-26

Ferdinand Omanyala amefichua kuwa mpenziwe amekuwa kiungo muhimu katika safari yake kabla ya kuwika kwenye mbio za mita 100.

Omanyala mwenye umri wa miaka 25 alisema alikuwa akiishi mtaani Huruma na mpenziwe kipindi cha Coronavirus bila kibarua.

Alisema alitumia kipindi hicho cha masaibu ya Coronavirus kufanya mazoezi kwa miezi sita bila hata kuwa na lengo lolote.

"Ilikuwa ni mwaka mgumu lakini ni kama bahati kwa sababu nilifanya mazoezi kwa miezi sita. Hatukuwa na pesa

"Asanti kwa mpenzi wangu kwa sababu hatukuwa na pesa, alikuwa akilipa bili kwa sababu alikuwa akifanya kazi," aliongeza Omanyala.

Pia soma

Kiambu: Ruto Aahidi Kumzawadi Mama Mjane, Watoto Wake KSh 1 Milioni Ili Wanunue Shamba

Alisema sasa mlango wake wa baraka umefunguka na mpenziwe atapata kila kitu kitamu atakachotaka.

Kampuni ya michezo ya Odibets ilimzawadi Omanyala gari jipya aina ya Harrier Jumatano Septemba 22.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZ4RyfZJmmZ6hkmKurbXKrq6aZZGgtq21z5pkm6Gcnnqvtcuip6ijpayubrrIppysp6SWeqex0Z2gp5memXqwucCnsJqkkWKutLHMmmWhrJ2h